Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:46

Tume ya uchaguzi nchini Mali imeanza kuhesabu kura katika uchaguzi wa Jumapili


Raia wa Mali akitumia haki yake kupiga kura

Serikali ya kijeshi ambayo ilichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwaka 2020 na 2021 iliahidi kufanya kura hiyo ya maoni kama sehemu ya mpito kuelekea demokrasia chini ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumanne

Nchi ya Mali ilianza kuhesabu kura siku ya Jumapili kufuatia kura ya maoni ya katiba ambayo utawala wa kijeshi na mataifa yenye nguvu ya kikanda wamesema itafungua njia ya uchaguzi nchini humo na kurudi kwa utawala wa kiraia.

Serikali ya kijeshi ambayo ilichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi mwaka 2020 na 2021 iliahidi kufanya kura hiyo ya maoni kama sehemu ya mpito kuelekea demokrasia, chini ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi. Matokeo ya awali yanatarajiwa kutolewa siku ya Jumanne.

Baadhi ya vifungu vinavyopendekezwa katika katiba mpya vilivyoandaliwa na baraza la mpito vinaleta utata huku watetezi wakisema wataimarisha taasisi dhaifu za kisiasa na huku wapinzani wakisema hatua hiyo itampa rais madaraka mengi.

Lakini mashirika ya kikanda na Umoja wa Mataifa wanaiona kura hiyo ya maoni kama jaribio muhimu la serikali ya kijeshi kuwa tayari kuendelea na kipindi cha mpito na kufanya mchakato wa kidemokrasia wa nchi nzima, hasa katika wakati ambapo wanamgambo wa Kiislamu wanazidisha mashambulizi.

Kwa mradi huu, tunabashiri juu ya mustakbali wa nchi yetu, kurejeshwa kwa mamlaka yake, na kurejesha uaminifu kati ya taasisi na raia, Rais wa mpito Kanali Assimi Goita alisema katika hotuba kwa njia ya televisheni Ijumaa.

Rasimu hiyo inajumuisha taarifa mpya ambazo zimependekezwa katika juhudi za zamani zilizofeli za kurekebisha katiba ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa bunge la pili ili kuongeza uwakilishi kutoka nchi yote ya Mali.

Forum

XS
SM
MD
LG