Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 10:37

Uchaguzi Marekani: Rubio ajitoa, Clinton na Trump waongeza kasi


Gavana wa Ohio John Kasich

Seneta Mrepublican Marco Rubio wa Florida amejitoa katika kuwania ugombea urais kwa chama hicho baada ya kushindwa kwenye jimbo lake wakati Gavana wa Ohio John Kasich amepata ushindi muhimu katika jimbo lake na kumpa nguvu mpya katika kinyang'anyiro kwa upande wa ware publican baada ya kura za awali Jumanne.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:05 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Donald Trump ambaye anaongoza kwa upande wa chama hicho alijiongezea kasi kwa kupata ushindi mkubwa katika jimbo la Florida, huku Seneta wa Texas Ted Cruz na Kasich wakiwa nyuma yake. Trump pia alishinda katika majimbo ya Illinois na North Carolina.

APTOPIX DEM 2016 Clinton
APTOPIX DEM 2016 Clinton

​Baada ya kushindwa katika jimbo lake, Rubio alisema anashukuru wote waliomwunga mkono, akiongeza kuwa haikuwa "mpango wa Mungu" kwa yeye kuwa rais mwaka 2016.

Ohio ni jimbo lenye wajumbe wengi katika mkutano mkuu wa uteuzi wa chama cha Republican hivyo ushindi wake unampa Kasich nguvu mpya katika kampeni yake. Akizungumza baada ya ushindi wake alibashiri kuwa atakuwa mshindani mkuu katika chaguzi zijazo za awali kuwania ugombea.

Kwa upande wa Wademokrat, Hillary Clinton alimshinda Seneta Bernie Sanders kwa kura nyingi katika majimbo muhimu ya Florida, North Carolina na Ohio na hivyo kuchukua wajumbe wengi kutoka majimbo hayo.

Clinton alisema Jumanne ilikuwa "Super Tuesday" nyingine kwake, na kumpa hongera Sanders kwa kile alichosema ni kampeni ya nguvu.

Clinton ameongeza sana idadi yake ya wajumbe kuelekea mkutano mkuu wa chama cha Democrat huku Sanders akiendelea kupambana vikali kujaribu kumpiku Clinton ingawa wachambuzi wengi wanasema bila shaka Clinton hatimaye atakuwa mgombea rasmi wa chama cha Democrat.

XS
SM
MD
LG