Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 22, 2025 Local time: 02:19

Kampuni ya Japan kuwekeza dola bilioni 50 Marekani


Rais mteule wa Marekani Donald Trump akiwa na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Softbank, Masayoshi Son.
Rais mteule wa Marekani Donald Trump akiwa na mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Softbank, Masayoshi Son.

Kampuni kubwa ya mawasiliano kutoka Japan ya Softbank group, inapanga kuwekeza dola bilioni 50 katika uchumi wa Marekani.

Kampuni kubwa ya mawasiliano kutoka Japan ya Softbank group, inapanga kuwekeza dola bilioni 50 katika uchumi wa Marekani na kuongeza nafasi elfu 50 za ajira. Rais mteule Donald trump alitangaza Jumanne. Trump alionekana kwenye jengo la Trump Towers na mtendaji mkuu wa Softbank, Masayoshi Son, akitangaza habari hiyo na kisha baadaye kuandika kwenye mtandao wake wa twitter.

Son hakusema ni uwekezaji gani ananuia kufanya. Wakati akiongea na waandishi wa habari, alikuwa ameshika kipande cha karatasi chenye tarakimu sawa na zile Trump alizotangaza, lakini pia ilifafanuliwa kuwa uwekezaji huo ungefanyika kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Jumanne jioni, Trump alitangaza rasmi uteuzi wa Jenerali mstaafu Jammes ‘mad dog’ Mattis kuwa waziri wa ulinzi.. Mattis amewahi kuhudumu kama mkuu wa kituo cha kamandi ya Marekani iliofanya operesheni za Marekani huko mashariki ya kati, na kamanda mkuu wa ushirika wa majeshi ya NATO.

XS
SM
MD
LG