Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 19:20

Trump kukutana na wabunge muhimu wa Michigan baada ya kushindwa mahakamani


Rais Donald Trump (kushoto) na rais Mteule Joe Biden (kulia)
Rais Donald Trump (kushoto) na rais Mteule Joe Biden (kulia)

Rais wa Marekani Donald Trump amewaalika wabunge muhimu wa chama cha Republican kutoka jimbo la Michigan kwa mkutano katika white house, leo ijumaa, baada ya kushindwa katika kesi alizofikisha mahakamani kupinga ushindi wa rais mteule Joe Biden.

Haijabainika kile ambacho Trump atawaambia wabunge hao wala idadi ya wabunge watakaoitikia mwito wake na kusafiri hadi Washington kwa mkutano huo.

Mawakili wa Trump waliachana na kesi walizokuwa wamewasilisha katika mahakama kupinga matokeo ya kura katika jimbo la Michigan.

Hatua ya Trump kuwaalika wabunge hao inajiri baada ya timu yake ya kampeni kushindwa katika kesi kadhaa walizowasilisha mahakamni katika majimbo ambayo Trump alishindwa.

Biden alishinda jimbo la Michigan kwa zaidi ya kura 150,000.

Kura 16 za jimbo la Michigan ni muhimu kwa ushindi wa kura za wajumbe 270 ambazo mshindi anastahili kupata.

Iwapo bodi ya uchaguzi ya Michigan haitaidhinisha matokeo ya kura za uchaguzi wa Nov 3 kufikia Jumatatu wiki ijayo, jimbo hilo ambalo kwa sasa linadhibitiwa na warepublican, litahitajika kuingilia kati na kuteua wafuasi wa Trump kuwa waamuzi wa kura 16 na kutupilia mbali kura za wapiga kura wa kawaida.

Hatua kama hiyo haijawahi kutokea katika historia ya uchaguzi wa Marekani katika siku za hivi karibuni.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG