Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 04:35

Trump kufika kwenye mahakama ya Washington Alhamisi


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Alhamisi anatarajiwa kufika mahakamani mjini Washington DC, ili kujibu mashitaka kutokana na tuhuma za kujaribu kubadili kushindwa kwake katika uchaguzi wa 2020.

Hali ya usalama imeimarishwa karibu na jengo la mahakama wakati wa kesi hiyo. Baadhi ya mambo anayotarajiwa kufanyiwa ni pamoja na kuchukuliwa kwa alama za vidole, pamoja na kukanusha mashitaka dhidi yake.

Jopo la mahakama wiki hii limemfungulia mashitaka manne ya uhalifu, ikiwa ni pamoja na njama ya kuilaghai Marekani, kuingilia kati mchakato rasmi, na njama za kuwanyima wapiga kura haki yao ya uchaguzi huru na wa haki.

Waendesha mashitaka wamesema kwamba Trump amerejea kudai kuwa kulikuwa na wizi katika uchaguzi wakati ambapo alifahamu kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli, huku akiwashinikiza maafisa wa uchaguzi pamoja na naibu wake wa Rais Mike Pence, wachukue hatua za kuhakikisha anabaki madarakani.

Forum

XS
SM
MD
LG