Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:53

Trump, Kim wako Singapore kuanza mazungumzo


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Dr Vivian Balakrishnan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi June 10, 2018.
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore Dr Vivian Balakrishnan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changi June 10, 2018.

Kim Jong Un Jumapili alikuwa mbali zaidi na makazi yake Korea Kaskazini kuliko wakati wowote tangu alipochukuwa madaraka 2011.

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliwasili nchini Singapore Jumapili mchana, akiwa amepanda ndege ya China iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Changi.

Kim siku ya Jumanne atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump katika mkutano wa kihistoria ambao Trump ameuita ni “ni fursa ya kipekee” katika kufikia amani.

Vyombo vya habari havikuweza kumuona Kim wakati alipokuwa akisindikizwa katika gari aina ya Mercedes-Benz limousine rangi nyeusi ambayo ilikuwa vioo vyake ni vya tinted, kutoka uwanja wa ndege kwenda kwenye hoteli ya kifahari ya St. Regis.

Watalii na makundi ya vyombo vya habari vya kimataifa, ambao wako Singapore kuripoti mkutano huu, walielekeza kamera zao, walitabasamu na kupungia mkono gari hilo, ambalo lilikuwa limezingirwa na walinzi wakakamavu wa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini wakikimbia pembeni ya gari lake.

Baadae, Kim alitokea kwa kujiamini na kutabasamu akizielekea camera wakati akiendelea kupeana mikono na waziri mkuu wa Singapore, Lee Hsien Loong, katika Ikulu ya Istana.

Trump ambaye aliwasili Singapore muda mfupi baada ya kuwasili Kim, atakutana na Waziri Mkuu Lee Jumatatu.

Singapore inaonekana kuwa ni mahali muafaka kwa mkutano huo - wa kwanza kabisa kuweza kufanyika kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani aliyeko madarakani.

XS
SM
MD
LG