Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:20

Trump asema mkutano wake na Kim hautafanyika


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump amesema mkutano wake na kiongozi wa Korea Kim Jong Un uliopangwa kufanyika Juni 12 huko Singapore hautafanyika.

“Nilikuwa na subiri kwa hamu kuwa pamoja na wewe,” Trump amesema katika barua aliyo muandikia Kim iliyotolewa na White House.

Barua hiyo imeeleza pia kuwa: “Kwa masikitiko, kutokana na kuonyesha hasira na uchokozi ulio wazi katika matamko yako ya hivi karibuni, nina hisi haistahili kwa wakati huu kuwa na mkutano huu uliopangwa muda mrefu.”

Kitu cha mwisho kilichoharibu mazungumzo haya, kwa mujibu wa afisa wa White House, ilikuwa ni tusi dhidi ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence mapema Alhamisi katika tamko la waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Choe Son Hui.

Mwanamke huyo alimwita Pence “ni karagosi la kisiasa” na kuonya kwa tamko la kisiasa kauli inayofanana na matamko ya Pyongyang ya malumbano juu ya silaha za nyuklia.

XS
SM
MD
LG