Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 17:01

Trump apiga kura

Rais Donald Trump akiwa amevaa barakoa aondoka kwa kituo cha kupigia kura mjini West Palm Beach Florida baada ya kupiga kura ya mapema Jumamosi Oktoba 24, 2020.
Rais Donald Trump akiwa amevaa barakoa aondoka kwa kituo cha kupigia kura mjini West Palm Beach Florida baada ya kupiga kura ya mapema Jumamosi Oktoba 24, 2020.

Rais Donald Trump wa Marekani, Jumamosi alipiga kura ya mapema kwenye kituo kimoja katika jimbo la Florida, katika wikendi ambayo yeye na mpinzani wake, Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden, waliendelea kuhudhuria na kuhurubia mikutano katika miji mbalimbali nchini, kunadi sera zao, kwelekea kwa uchaguzi wa tarehe tatu mwezi ujao.

Trump, ambaye mwaka jana alibadilisha makazi yake rasmi kutoka new York hadi Florida, alipiga kura mwendo wa asubuhi katika mji wa West Palm Beach.

Alipoulizwa na waandishi wa Habari ni nani aliyempigia kura, Trump alisema: "Nimempigia kura jamaa mmoja anayeitwa Trump," na kuongeza kwamba "ni heshima kwangu kuweza kupiga kura.”

Biden naye amekita kambi katika jimbo lenye ushindani mkubwa la Pennsylvania ambako amehutubia wafuasi wake na kumshutumu rais Trump kwa jinsi alivyolishughulikia suala la janga la Corona.

Rais Donald Trump, akiwa amevaa barakoa, atoka kwenye kituo cha kupigia kura cha West Palm Beach, Florida Jumamosi Oktoba 24,2020.
Rais Donald Trump, akiwa amevaa barakoa, atoka kwenye kituo cha kupigia kura cha West Palm Beach, Florida Jumamosi Oktoba 24,2020.

Trump anaelekea mjini Lumberton N Carolina, kwa mkutano wa kampeni, na baadaye kwenye majimbo ya Ohio na Wisconsin.

Utafiti wa maoni unaonyesha kwamba bado kuna ushindani mkubwa kwenye baadhi ya majimbo, licha ya kwamba tayari zaidi ya Wamerakani milioni 50 walikuwa wamepiga kura za mapema kufikia Jumamosi asubuhi.

XS
SM
MD
LG