Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 01:06

Trump aondolewa ghafla na maafisa wa 'Secret Service' baada ya mtu kupigwa risasi karibu na White House


Rais wa Marekani Donald Trump akiondoka gahfla kwa chumba cha kuwahutubia waandishi wa habari ndani ya ikulu mjini Washington DC Jumatatu tarehe 10, Agosti 2020. REUTERS/Kevin Lamarque
Rais wa Marekani Donald Trump akiondoka gahfla kwa chumba cha kuwahutubia waandishi wa habari ndani ya ikulu mjini Washington DC Jumatatu tarehe 10, Agosti 2020. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump, Jumatatu jioni kwa ghafla aliondolewa na maafisa wanaolinda usalama wake, kutoka kwenye chumba alimokuwa akiwahutubia waandishi wa habari ndani ya Ikulu mjini Washington, kufuatia kisa cha mtu kupigwa risasi karibu na ikulu hiyo.

Trump alikuwa tu ameanza kusoma hotuba yake wakati afisa mmoja wa idara ya Secret Service, alipomkaribia na kumnong’onezea, na kiongozi huyo akaondoka kwenye jukwaa na kuwaacha waandishi wa habari chumbani humo bila kusema chochote.

Kulikuwa na hali ya wasiwasi huku wanahabari wakijaribu kufahamu ni nini kilikuwa kimetokea.

Dakika chache baadaye, rais huyo alirejea na kuwaambia waandishi hao kwamba kulikwa na kisa ambapo mtu mmoja alipigwa risasi na maafisa wa usalama nje kidogo ya ikulu.

Alisema mtu aliyejeruhiwa alikuwa hospitalini, na kuongeza kwamba hali ilikuwa imedhibitiwa.

Baadaye, maafisa wa kulinda usalama wa rais walituma ujumbe kupitia mtandao wa Twtter na kuthibitisha kwamba afisa mmoja alimpiga risasi mtu mmoja karibu na White House.

"Kisa hicho cha kilitokea kwenye makutano ya barabara za Pensylvania Avenue na 17th," ujumbe huo wa Twitter ulieleza.

Idara hiyo ilisema maelezo Zaidi yatatolewa baadaye.

XS
SM
MD
LG