Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 00:54

Trump anaendelea kuwashambulia vigogo waliokataa kumuunga mkono


Mgombea urais wa Republican hapa nchini, Donald Trump.
Mgombea urais wa Republican hapa nchini, Donald Trump.

Mgombea urais wa Republican nchini Marekani, Donald Trump alisema huwenda yupo kwenye nafasi nzuri bila ya kupata uungaji mkono wa watu dhaifu ndani ya chama chake akiwemo spika wa bunge Paul Ryan.

Trump alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Fox News cha Marekani kwamba Ryan na wanachama wengine bungeni walikuwa hawampendi na kukataa kumuunga mkono katika ugombea wake wa urais.

Matamshi hayo yamekuja siku kadhaa baada ya kutolewa mkanda wa video uliorekodiwa mwaka 2005 ambapo Trump alitoa matamshi mabaya kuhusu kuwadhalilisha wanawake na kupelekea wabunge kadhaa wa chama cha Republican kusema hawatamuunga mkono katika harakati zake za kuingia White House.

Mgombea huyo alisema kwenye mtandao wa Twitter kwamba ni vizuri kuona kwamba wale wasionitaka wamejitoa na hivi sasa ninaweza kuwapigania wamarekani kwa namna ninavyotaka kuendesha kampeni yangu.

XS
SM
MD
LG