Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 12:50

Trump ametumia amri ya utendaji kusitisha familia kutengana


Trump akionesha saini ya amri ya utendaji. June 20, 2018.
Trump akionesha saini ya amri ya utendaji. June 20, 2018.

Rais Donald Trump wa Marekani alibaedili msimamo wake siku ya Jumatano na kutia saini amri ya utendaji inayositisha hatua ya kuzitenganisha familia na watoto wao wanapoingia Marekani kinyume cha sheria kwenye mpaka na Marekani na Mexico. Hata hivyo amesisitiza kwamba amri hiyo haitobadili sera yake ya kutowastahmilia wahamiaji wanaojaribu kuingia Marekani kinyume cha Sheria.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuna mambo kadhaa yaliyomsababisha kuchukua hatua hiyo kwanza inabidi kutaja hapa kwamba Trump tangu alipochukua madaraka na hata kabla hapendi kubadili misimamo au hatua anazochukua.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mchambuzi wa masuala ya uhamiaji Dr. Timothy Sadera wa jimbo la Georgia, Marekani na kwanza kumuuliza hatua hiyo ina maana gani kwa watoto na wazazi vile vile changamoto zake ni zipi kwa jamii.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:29 0:00

Sasa wachambuzi wanasema mabadiliko ya Jumatano huwenda kwanza yanatokana na mkewe Melania Trump ambaye mapema wiki hii kupitia msemaji wake alisema haungi mkono zoezi la kuwatenganisha watoto na wazazi wao, baada ya matamshi ya wake watatu wa marais wa zamani wa Marekani kusema matamshi kama hayo akiwemo Michelle Obama, Hillary Clinton na Laura Bush. Pia kuna kilio kikubwa cha kisiasa kutoka kwa wahafidhina na viongozi wa makanisa wanaomuunga mkono mbali na ukosowaji mkali kutoka kwa wa-Democrats na wa-Republican kwa ujumla na viongozi wa kigeni pamoja na Papa Francis.

Rais Trump (C) na Makamu Rais Mike Pence na waziri Kirstjen Nielsen
Rais Trump (C) na Makamu Rais Mike Pence na waziri Kirstjen Nielsen

Rais Trump baada ya mkutano na baraza lake la mawaziri huko White House akiwa pamoja na Makamu Rais, Mike Pence na waziri wa usalama wa ndani Kirstjen Nielsen alitia saini amri ya utendaji na kusema “Hii inahusu kuweka familia pamoja, huku wakati huo huo inahakikisha kwamba tuna usalama thabiti kabisa wa mpakani, na usalama wa mpakani utakua kama ulivyokuwepo au hata kuimarishwa zaidi”.

Chini ya amri hiyo wizara ya usalama wa ndani itazishikilia pamoja familia za kigeni zilizoingia huku utaratibu wao wa kisheria kuhusu kuingia kiunyume cha sheria unashughulikiwa. Amri inaamrisha pia wizara ya ulinzi kutowa mahala au kujenga mahala ambako familia hizo zitashikiliwa. Na wizara ya sheria imetakiwa kwa uwezo wake kuweka kipau mbele utekelezaji wa kesi zinazohusu familia zinazoshikiliwa.

Rais Trump ambae pamoja na maafisa wa serikali yake wamekua kwa siku kadhaa wakishikilia kwamba hawawezi kuchukua hatua peke yao kubadili utaratibu huo bila ya idhini ya bunge, alisema sera jumla ya kutostahmilia kabisa wahamiaji kuingia kinyumke cha sheria haitobadilika. “Sikupenda kile nilichokua nakiona pale familia zikitaabika wanapotenganishwa. Ni tatizo ambalo limekua likiendelea kwa miaka mingi kama mnavyofahamu kupitia utawala mbali mbali, na sisi tunafanya kazi kuleta mabadilkiko katika mfumo wa uhamiaji”.

XS
SM
MD
LG