Jaji wa mahakama hiyo amesema hayo yalijiri licha ya kuambiwa kuwa nambari hizo sio sahihi.
Jaji wa mahakama moja David Carter alifichua hayo akimwamuru wakili John Eastman kutoa barua pepe zaidi kwa kamati ya bunge inayochunguza shambulio la Januari 6, 2021 dhidi ya bunge la Marekani la wafuasi wa Trump.
Eastman alikuwa mmoja wa mawakili wa Trump wakati rais huyo wa zamani na washirika wake walipopinga kushindwa kwake katika uchaguzi wa mqwaka 2020 na Joe Biden.
Wawakilishi wa Trump na Eastman hawakujibu mara moja maombi ya maoni yao.
Carter alisema Jumatano kwamba Trump "alitia saini uthibitisho wa kiapo" kwamba nambari zisizo sahihi za udanganyifu ni za "kweli na sahihi" au "zinaaminika kuwa za kweli na sahihi" kwa kadri ya ufahamu na imani yake, wakati akidai kuhesabiwa vibaya kwa kura katika kaunti moja huko Georgia.