Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:57

Trump ageukia sheria muhimu za usimamizi wa fedha


Rais Donald Trump akionyesha amri ya kiutendaji inayoondoa sheria ya Dodd-Frank
Rais Donald Trump akionyesha amri ya kiutendaji inayoondoa sheria ya Dodd-Frank

Rais Donald Trump amechukua hatua za kuziondoa sheria muhimu za usimamizi wa masoko ya fedha, ikiwemo ile sheria ya Dodd-Frank iliyokuwa imewekwa kuzuia migogoro ya mabenki.

Hata hivyo Sheria ya Dodd-Frank ilikuwa inasimamia hatua za kuwataka washauri wa kifedha kuchukua hatua zinazolinda zaidi maslahi ya wateja wake.

“Leo, tunasaini misingi muhimu ya usimamizi wa mifumo ya kifedha nchini Marekani,” Trump amesema Ijumaa. “Haziongezeki zaidi ya hizi.”

Uongozi wa Obama ulikamilisha hatua za kuleta mabadiliko Wall Street ambazo zinajumuisha taasisi zinazosimamia mifumo ya fedha baada ya kuyumba kifedha 2008.

Trump akosoa

Lakini uongozi wa Trump umekosoa kanuni zilizowekwa na kusema kuwa hazimlindi mlaji kama inavyotakiwa, na kuwa ni mzigo mkubwa na zinazuia uzalishaji.

Uongozi huo utaanza “kuondoa vipengele vingi katika sheria ya Dodd-Frank kwa sababu kiukweli nina watu wengi, marafiki zangu wanabiashara nzuri. Hawawezi kukopa pesa benki kwa sababu ya vizuizi vingi,” Trump amesema.

Katika amri ya kiutendaji, Trump ameamuru kupitiwa sheria hizo na kanuni ambazo zinasimamia mifumo ya kifedha Marekani katika juhudi za kuondoa sheria ya marekebisho ya fedha 2010, inayojulikana kama Dodd-Frank.

Juhudi ya Obama

Kutoka kushoto: Rais Donald Trump na Rais mstaafu Barack Obama
Kutoka kushoto: Rais Donald Trump na Rais mstaafu Barack Obama

​Wachambuzi wa kisiasa wamesema kuwa amri hiyo ya kufumua sheria za usimamizi wa taasisi za fedha ni hatua ya Trump kutekeleza ahadi aliyotoa wakati wa kampeni kuwa ataiondosha hiyo sheria, inayojulikana kama Dodd-Frank.

Marekebisho yaliyokuja kujulikana kama sheria ya Dodd-Frank ya marekebisho ya Wall Street na kumlinda mlaji ni ya uongozi wa rais mstaafu katika kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi ulioikumba Marekani mwaka 2008.

Lengo kubwa la sheria hii ni kupunguza hatari katika mifumo ya kifedha kwa kuweka wakala mbalimbali.

Trump pia amesaini amri nyingine ya kiutendaji ikiiagiza Wizara ya Kazi kupitia sheria inayojulikana kama utawala wa maadili yaani 'fiduciary rule' ambayo ingeanza kutumika Aprili.

Amri hiyo kisheria inawataka washauri wa kifedha kuweka maslahi ya wateja wao mbele ya maslahi yao binafsi.

White House imeahidi kubadilisha kanuni za fedha kwa namna ambayo itaongeza ajira na kuwalinda walaji.

XS
SM
MD
LG