Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 19:46

Trump apendekeza hukumu ya kifo kwa walanguzi wa dawa za kulewa


Rais wa Marekani Donald Trumpakitoa hituba huko Manchester New Hampshire juu ya kupambana na tatizo la matumizi mabaya ya madawa, Machi 19, 2018.
Rais wa Marekani Donald Trumpakitoa hituba huko Manchester New Hampshire juu ya kupambana na tatizo la matumizi mabaya ya madawa, Machi 19, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa mpango wake uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu wa kupambana na matumizi ya madawa ya kutuliza maumivu kupita kiasi Jumatatu .

Katika hotuba kwenye mkutano huko Manchester New Hampshire Trump aliahidi kuwepo na kizazi kisichotumia madawa akisema kwa pamoja tutamaliza janga hili la ulevi wa dawa hapa Marekani moja kwa moja.

Trump amesema ili kushinda inabidi kuwa mkali kwa wauza dawa za kulewa.

"Kama tusipokuwa wakali kwa wauza madawa tunapoteza muda wetu”.Na ukali huo ni pamoja na adhabu ya kifo aliongeza huku waliokuwa wakimsikiliza wakimpigia makofi.

Kiongozi wa walio wachache bungeni Nancy Pelosi ameonya kwamba mapendekezo ya rais yanahitaji fedha au yataishia kuwa ahadi hewa kutoka utawala wake.

Bajeti ya Trump ilipendekeza makato makubwa fedha za huduma kwa wazee,idara ya magonjwa ya kuambukliza , magonjwa ya akili na utumizi mbaya wa madawa ambao ulikuwa ni muhimu kusaidia familia zinazopambana na matumizi mabaya ya madawa hayo ya kutuliza maumivu. Amefanya kazi kuharibu mpango wa afya wa gharama nafuu na kuruhusu uuzaji wa bima isiyo na faida kwa wengi ambayo haihudumii walioathirika na madawa. Na sasa Rais Trump anazungumzia kuweka adhabu ya kifo kwa makosa ya madawa" Pelosi alisema.
Bado haijafahamika ni jinsi gani waendesha mashitaka wanaweza kuomba adhabu ya kifo bila kubadili sheria za Marekani baadhi ya wasomi wa sheria wanasema jambo hilo huenda ikabidi kuamuliwa na mahakama ya juu ya Marekani.

XS
SM
MD
LG