Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 19:09

Siasa za kuvunjwa kwa Tume ya IEBC zaendelea Kenya


Orange Democratic Movement leader Raila Odinga addresses the crowd during a rally at Uhuru Park in Nairobi, July 7, 2014.
Orange Democratic Movement leader Raila Odinga addresses the crowd during a rally at Uhuru Park in Nairobi, July 7, 2014.

Swala la shinikizo la kuvunjwa kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC huko Kenya limekuwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo vya habari hasa baada ya maandamano yaliyofanywa na wafuasi wa CORD wakiongozwa na Raila Odinga hadi makao makuu ya IEBC.

Ripoti mpya iliotolewa Jumatano kwenye gazeti la Standard inasema kuwa kando na muungano wa CORD, wagombea kiti cha rais kwenye uchaguzi mkuu uliopita pia wanalalamika kuhusu tume hiyo ya uchaguzi. Wagombea Musalia Mudavadi, Peter Kenneth, Martha Karua na James ole Kiyiapi wanasema kuwa tume ya uchaguzi inahitaji marekebisho.

Swala hili kwa hakika limechochea maoni mengi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari. Kwenye gazeti hilo hilo la Standard, Railka Muodho anasema kuwa anashuku mwandishi wa ripoti hiyo. Inakuwaje viongozi hao wote wametoa maoni yao wakati mmoja?

Kumuseno anasema kuwa vyombo vya habari visilaumiwe kwa kuchapisha ripoti hiyo. Vinafanya kazi yao tu. Sanity kwa upande wake anasema kuwa Raila anafaa kutafutiwa kazi kwani anachochea wafuasi wake kutokana na upweke Thruthru nae anaongeza kuwa tume hiyo inafaa kuvunjwa ili Kenya ikaanza upya.

XS
SM
MD
LG