Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:42

Transnet ya Afrika kusini yatangaza hatua za dharura kufunga eneo la bandari la Richards Bay


Mfano wa kazi zinazofanywa na Transnet katika bandari ya Afrika kusini
Mfano wa kazi zinazofanywa na Transnet katika bandari ya Afrika kusini

Hatua hii inafuatia tukio la moto uliozuka Jumatano. Richards Bay Bulk Terminal ni kituo kikubwa sana barani Afrika cha kusafirisha  makaa ya mawe kinapatikana kwenye bandari hiyo ya Richards Bay moja ya bandari saba za kibiashara ambazo Transnet inaziendesha kwenye pwani ya Afrika kusini

Msimamizi pekee wa bandari ya Afrika kusini, Transnet, Ijumaa alitangaza kuchukua hatua za dharura kufunga eneo la “Richards Bay Bulk Terminal”, ilisema taarifa kufuatia moto uliozuka bandarini Jumatano.

Richards Bay Bulk Terminal ni kituo kikubwa sana barani Afrika cha kusafirisha makaa ya mawe kinapatikana kwenye bandari hiyo ya Richards Bay moja ya bandari saba za kibiashara ambazo Transnet inaziendesha kwenye pwani ya Afrika kusini.

Transnet haikusema ikiwa au kwa kiasi gani mauzo ya bidhaa kama makaa ya mawe, chuma, na madini mengine yataathiriwa. "Kituo kinashirikiana na wateja wake walioathirika, na kipo katika mchakato wa kuweka dharura zinazohitajika kwani njia nyingine zinafanya kazi", kampuni hiyo inayomilikiwa na serikali ilisema katika taarifa iliyotolewa Ijumaa usiku.

XS
SM
MD
LG