Timu ya wafanyakazi kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa duniani IMF inazuru Kenya kwa safari ya kutafuta ukweli, IMF ilisema Alhamisi jioni ikiwa sehemu ya juhudi za kuandaa namna ya kusonga mbele kufuatia maandamano mabaya ambayo yaliondoa ongezeko la kodi lililopangwa na serikali.
Rais William Ruto alitupilia mbali muswaada huo wa fedha wa mwaka mwezi Juni, na hivyo kuacha serikali ikiwa na deni kubwa na nakisi kubwa ya bajeti ya mwaka huu wa kifedha, na kuongezeka madeni bili ambayo hayajalipwa, na kucheleweshwa kwa fedha za ufadhili wa IMF.
Hii ni dhamira ya kutafuta ukweli na ni sehemu ya mazungumzo yetu yanayoendelea na yenye kujenga na serikali ya Kenya ili kutafuta njia iliyo bora kuelekea mbele Julie Kozack, mkuu wa mawasiliano wa IMF, aliambia kikao cha wanahabari.
Forum