Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 15:58

Timu ya Rwanda Energy Group (REG) imekuwa ya kwanza kufuzu kwenda fainali za BAL


Jean Jacques wa REG akikimbia na mpira huku akifuatwa na Oussama Marnaoui wa US Monastirienne Machi 14, 2022. GETTY

Timu ya Rwanda Energy Group (REG) imekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali za ligi ya mpira wa kikapu Afrika mwezi Mei huko Rwanda baada ya kuifunga AS Douanes ya Senegal kwa jumla ya pointi 69-55 katika kanda ya Sahara mjini Dakar, Senegal, Jumatano.

Katika kuelekea ushindi wake wa tatu wa kanda hiyo REG walianza kwa nguvu na alikuwa ni mchezaji Ndizeye akipachika point tatu baada ya kupokea pasi kutoka kwa Cleveland Thomas Jr.

Dieudonné Ndizeye ambaye alianza mchezo huo kwa nguvu alipachika pointi tatu nyingine katika sekunde za mwisho za kota ya kwanza na kuipa REG uongozi wa pointi tano.

Wilson Nshobozwa naye alipachika pointi nyingine tatu wakati kota ya tatu inapomalizika na kuiweka REG pointi kumi mbele.

Nao ASA Douanes walipachika vikapu viwili vya haraka haraka ikiwa ni pamoja na mpira uliorushwa na Marcus Crawford baada ya Cheikh Kamara kuchukua mpira.

Vijana wa REG walisukuma mashambulizi ya kasi katika kota ya tatu baada ya kukosa nafasi kwa Dali Fall wa AS Douanes . Pasi mbili ndefu zinampa nafasi mchezaji wa REG Ndizeye kufunga pointi kwa urahisi na kuongeza uongozi wa REG.

AS Douanes walipambana vikali na kukata uongozi wa pointi 21 wa REG kwa danki ya nguvu ya Victor Diagne.

Lakini REG walionekana kuwazidi sana timu ya Senegal wakati Ulrich Chomche alipofunga pointi kwa mpira wa kuvutuia akiwa nje ya mstari wa mipora ya adhabu na kuiweka juu timu ya Rwanda isifikiwe na wapinzani wao kwa ushindi wa jumla ya poiti 69-55.

Huku wakiwa na michezo miwili mkononi katika kanda hiyo timu hii ya Rwanda ina uhakika wa kucheza mechi za fainali huko nyumbani Rwanda mwezi Mei.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG