Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:56

Mjue Tim Kaine mgombea mwenza wa Hillary Clinton


Tim Kaine, mgombea mwenza wa Mdemocrat HIllary Clinton.
Tim Kaine, mgombea mwenza wa Mdemocrat HIllary Clinton.

Mgombea urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton alipomchagua Tim Kaine kama mgombea mwenza wake, seneta wa Virginia alikuwa wa kwanza kukiri kuwa hajulikana sana ndani ya chama cha Democratic.

Kinyume na wagombea wawili wa urais, Clinton na Donald Trump, kufahamika sana kwa kubainisha majibu yenye nguvu, Kaine mara kwa mara anaelezewa kuwa ni ‘mtu mzuri’ katika siasa.

Kinyume na mgombea mwenza wa Trump, Mike Pence, ambaye ametumia muda mwingi kuomba msamaha kwa kuelezea misimamo ya Trump, Kaine amejaribu kuwavutia wapiga kura na kuvutia mwelekeo chanya kwa Clinton.

Amekuwa akijihusisha na wapiga kura waspanish baada ya kutumia muda mwingi huko Amerika ya Kati,, na pia kuwafikia wapiga kura wa Mormoni huko Utah kutokana na kazi yake kama mmishionari, na amejaribu kuwafikia pia warepublican kama mdemocrat mwenye msimamo wa wastani.

Timothy Michael ‘Tim’ Kaine alizaliwa februari 26, 1958, huko st. paul Minnesota, lakini alikulia Kansas city, Missouri. Ni mtoto mkubwa wa mfanyakazi wa kiwanda na mwalimu.

Kaine alihudhuria shule ya sekondari ya wavulana Jesuit, ambako alijiunga na harakati za Jesuit nchini Honduras. Alipata shahada ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Missouri kabla kuingia shule ya sheria ya Havard.

Kaine aliacha masomo ya sheria kwa muda ili kwenda kufanya kazi na Jesuit Volunteer Corps nchini Honduras kwa miezi tisa mwaka 1980 mpaka 1981, akisaidia wamishionari wa Jesuit ambao walikuwa wakiendesha shule ya kikatoliki huko El Pregreso.

Wakati alipokuwa huko alisaidia kuwaunga mkono wahamiaji wasio na makaratasi walioko nchini Marekani, msimamo ambao huenda ukawavutia wapiga kura walatino. Pia alijifunza kispanish, na hiyo inaonekana kuwa itawavutia wapiga kura waspanish.

Kaine alikutana na mkewe, Anne Holton, kwenye shule ya sheria ya Havard. Ni mtoto wa gavana wa zamani wa Virginia, Linwood Holton (1970 – 74), mrepublican ambaye alimaliza ubaguzi katika shule za umma kwenye jimbo hilo. Mke wake hivi sasa ni katibu wa elimu katika jimbo hilo. Wana watoto watatu, wakiume Nat na Wood na wa kike Annella.

Baada ya kuhitimu sheria, Kaine alihamia Richmond, Virginia, ambako alitumia muda wa karibu miongo miwili kutumika kama mwanasheria akilenga masuala ya haki za kiraia. Alisaidia kuanzisha ushirika wa Virginia kumaliza tatizo la watu wasiokuwa na makazi na alikuwa mwanachama wa Housing Opportunities Made Equal huko Virginia.

Aliingia katika siasa mwaka 1994 wakati alipochaguliwa katika baraza la mji la Richmond na baadaye kuwa meya.

Mwaka 2006 mpaka 2010 alikuwa gavana wa Virginia. Alichaguliwa katika baraza la senate 2012, baada ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya chama cha Democratic.

Clinton alipomtangaza mgombea mwenza wake, Jeff Flake, seneta mrepublican kutoka Arizona aliandika katika mtandao wake wa twitter:”najaribu kuangalia jinsi ya kumchukia Tim Kaine. Sina hata moja, hongera kwa mtu mzuri na rafiki mzuri.

XS
SM
MD
LG