Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 29, 2023 Local time: 17:47

Tigray yakaidi serikali kuu Ethiopia na kufanya uchaguzi


 Wananchi wakipiga kura katika mkoa wa Tigray September, 9, 2020 VOA/Mulgeta Atsbaha
Wananchi wakipiga kura katika mkoa wa Tigray September, 9, 2020 VOA/Mulgeta Atsbaha

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa Jumatano katika mkoa wa kaskazini mwa Ethiopia wa Tigray kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge, hatua inayopingana na serikali kuu. Kura hiyo ni changamoto ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu Abiy Ahmed, ambaye aliahirisha uchaguzi huo mkuu mapema mwaka huu kwa sababu ya janga la COVID-19. Chama cha Uhuru cha Tigray, kilichoanzishwa baada ya uchaguzi wa Ahmed mwaka 2018, kinashinikiza kujitenga na Ethiopia,

Uchaguzi katika eneo hilo ni swala ambalo limeisumbua serikali ya Waziri Mkuu Abiy wakati anajaribu kubadilisha nchi hiyo kuingia katika enzi mpya ya uwazi zaidi. Eneo la Tigray, ambalo liliongoza umoja wa serikali ya vyama vingi kwa miaka 27 kabla ya Abiy kuingia madarakani, lilipinga vikali uamuzi wa serikali mnamo mwezi Machi kuahirisha uchaguzi wa kitaifa kwa sababu ya corona. Imeita jaribio lolote la kuzuia kura yake ya kikanda kuendelea kama tamko la vita.

Lakini wakosoaji wa uchaguzi katika eneo la Tigray wanasema watawala wa zamani wa nchi hiyo wanatumia tu kura hiyo ili kuendeleza masilahi yao katika siasa za kitaifa na kutoa hasira zao kwani hawako tena madarakani.

“TPLF na baadhi ya wazalendo wa Tigray wanazungumza juu ya kujitangazia uhuru. Sidhani kama itakuwa hivyo. Badala yake, wanatengeneza hali itakayo imarisha madai yoyote waliyonayo katika siasa za kitaifa. Sidhani Tigray itajitenga na Ethiopia yote alisema Asnake Kefale, profesa katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa, alipozungumza na VOA kupitia App ya mtandao.

Asnake pia alielezea maoni yake kwamba Ethiopia inaweza kuanguka kama kikaragosi na akasema kwamba watu wamesahau kuwa watu hao hao wanaoandaa kura huko Tigray ni watu wale wale ambao waliongoza serikali ya ukandamizaji iliyofanya unyanyasaji wa haki za binadamu kwa watu wake.

Ni taasisi ya Ki-Marxist na -Lenin ambayo haikuruhusu ushindani wowote katika miaka 27 iliyopita. Wao wamekasirika sana kwa sababu walisukumwa kando”aliongeza.

Chama cha Uhuru cha Tigray, ambacho kilianzishwa mnamo mwezi Juni, kinasema kujitenga kabisa kutoka Ethiopia ndio lengo lake kuu.

Kiongozi wa chama hicho Girmay Berhe aliambia VOA kwamba alitarajia kwamba chama chake kitapata viti vyake vya kwanza katika bunge la mkoa. Alisema pia anafikiria uchaguzi huo utatoa majibu kutoka kwa serikali kuu, labda kwa kushinikiza watu wasiwekeze katika eneo la Tigray, au kwa kuchochea mvutano kati ya mikoa ya Amhara na Tigray.

Girmay ameongeza kuwa baada ya uchaguzi serikali kuu inaweza kushindwa kutambua uhalali wa serikali ya mkoa wa Tigray, hali ambayo alisema inaweza kuchochea wito wa uhuru kamili.

Katika hali hii, serikali ya Tigray inaweza kuanza kufanya kama serikali iliyojitenga. Kulingana na ni mambo gani yanayotokea baada ya hapo, kuna uwezekano wa Tigray kujitangazia uhuru. Tutakuwa tukishinikiza ajenda hii.” Alisisitiza Girmay.

Usiku wa kuamkia uchaguzi wa Tigray, Waziri Mkuu Abiy alisema kura hiyo kuwa ni mzunguko tu na akasema kutoshiriki kwa mkoa huo katika uchaguzi ujao wa kitaifa kutaifanya serikali ya mkoa huo kuwa si halali kabisa.

XS
SM
MD
LG