Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:37

Thamani ya Shilingi ya Kenya Yashuka


Bei ya bidhaa za kimsingi yapanda nchini Kenya
Bei ya bidhaa za kimsingi yapanda nchini Kenya

Wakenya wakabiliwa na ugumu wa maisha

Thamani ya sarafu ya Kenya Shilingi, imeshuka sana katika historia yake ikilinganishwa na dola ya Kimarekani katika muda wa wiki moja iliyopita na kusababisha ongezeko kubwa la bei ya vyakula na bidhaa za kimsingi.Hali hii imewafanya raia wengi wa Kenya na hata wafanyibiashara kushindwa kumudu bei za bidhaa.Dola moja ya Marekani wiki hii inabadilishwa kwa shilingi mia moja na mbili, ikilinganishwa na shilingi 80 mapema mwaka huu. Mfumko wa bei umefikia asili mia 16. Katika masoko mjini Nairobi wenye maduka wameanza kuathiriwa na mfumko huo wa kifedha. Bei za bidhaa za kimsingi zimepanda zaidi ya maradufu.Mtaalam wa maswala ya kiuchumi nchini Kenya Robert Shaw anasema sababu mojawapo ya kushuka kwa thamani ya shilingi ya Kenya ni ongezeko la bei ya mafuta yanayoagizwa kutoka nchi za nje pamoja na bidhaa nyingine. Lakini Benki kuu ya Kenya imeyumbayumba katika kulitafutia suluhu swala hilo ikilaumu benki za kibiashara kwa kuhodhi fedha za kigeni. Benki hiyo kuu sasa inapendekeza kuuzwa kwa fedha za kigeni kwa bei iliyopunguzwa kwa wafanyibaishara katika sekta ya uchumi kama wale wanaonunua mafuta kutoka nje. Lakini kwa wananchi wa kawaida wa Kenya wanashuku kuwa matajiri na wenye madaraka wanahodhi dola za kimarekani kujiandaa kwa uchaguzi ujao wa mwaka wa 2012 huku raia wengi wakishindwa kumudu bei ya vyakula vya kimsingi.

XS
SM
MD
LG