Wafanayakazi hao waliokolewa kutoka vituo vilivyokua vinafanya utapeli wa mitandao huko Myanmar.
Kundi la wanamgambo wa kibudha DKBA linasema liko tayari kuwakabidhi kwa jeshi la Mnyanmar zaidi ya watu 400 wanaodaiwa ni wafanyakazi wa vituo hivyo wengi wao kutoka nchi za Afrika, ili kurudishwa makwao.
Mkuu wa utawala wa DKBA amewaambia waandishi habari kwamba tatizo kubwa ni kwamba jeshi haliko tayari kuwapokea na kuwasafirisha nyumbani.
Wafanyakazi hao wanaosema walirubuniwa kwenda kufanya kazi katika vituo hivyo vya utapeli kwenye wilaya ya Myanmar inayopakana na Thailand ni raia wa karibu mataifa 22 na wengi wao ni kutoka Ethiopia.
Forum