Maelfu ya wanavijiji katika milima ya kaskazini magharibi mwa Nepal walilala nje usiku wa Jumamosi katika baridi kali, baada ya tetemeko la ardhi kuua watu wasiopungua 157 na kuziharibu nyumba nyingi.
Watu walitumia ubunifu walioweza kutengeneza makazi ya muda kwa usiku huo, kwa kutumia karatasi za plastiki na nguo za zamani ili kuwaweka kwenye hali ya joto.
Nyumba nyingi kwenye vijiji katika wilaya ya Jajarkot ama zilianguka au ziliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi la ghafla lililotokea Ijumaa usiku, huku nyumba chache zilizokuwa na misingi imara ya zege katika miji pia ziliharibiwa.
Watu wengi wameshindwa kuzipata mali zao kwa kuwa zimefukiwa chini ya kifusi. Serikali inajaribu kutoa misaada kwa maeneo yaliyoathirika.
Forum