Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 12:48

Tetemeko kubwa la ardhi latikisa Italia na kuua watu kadhaa


Mwili wa Mwathiriwa waondolewa kutoka kwa vifusi mjini Amatrice, Italia, baada ya tetemeko la ardhi lililotokea nchini homo siku ya Jumatano Agosti 24, 2016.
Mwili wa Mwathiriwa waondolewa kutoka kwa vifusi mjini Amatrice, Italia, baada ya tetemeko la ardhi lililotokea nchini homo siku ya Jumatano Agosti 24, 2016.

Tetemeko kubwa la ardhi lilitokea kati kati ya Italy mapema Jumatano na kusababisha uharibifu mkubwa kwenye maeneo karibu na makutano ya miji na kuuwa watu wasiopungua 39.

Idara ya hali ya hewa ya marekani imetaja tetemeko la kiwango cha 6.2 rikta kilichoanzia kwenye makutano ya kiasi cha kilomita 10 kusini-mashariki mwa mji wa Norcia.

Mtikisiko ulikumba sehemu kubwa ya eneo ikiwemo mji mkuu, Rome uliopo umbali wa kilomita 150. Mtetemeko ulianza baada ya saa tisa na nusu alfajiri kwa saa za huko na kufuatiwa na mitetemeko kadhaa baada ya hapo.

Idara ya kiraia ya kulinda majanga nchini Italy imesema watu kadhaa walijeruhiwa na wengi wanahitaji msaada wa makazi ya muda.

XS
SM
MD
LG