Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:18

Tetemeko jingine la ardhi lauwa watu 3 Uturuki


Maafisa wa kikosi maalum cha polisi wa Uturuki wakimbeba mwanaume aliyejeruhiwa baada ya tetemeko huko Antakya, katika mkoa wa Hatay, Februari 20, 2023.
Maafisa wa kikosi maalum cha polisi wa Uturuki wakimbeba mwanaume aliyejeruhiwa baada ya tetemeko huko Antakya, katika mkoa wa Hatay, Februari 20, 2023.

Tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 6.4 limeua watu watatu Jumatatu na kujeruhi wengine zaidi ya 200 katika baadhi ya maeneo ya Uturuki yaliyoharibiwa wiki mbili zilizopita na tetemeko kubwa lililoua maelfu ya watu, maafisa wamesema.

Majengo zaidi yaliporomoka, na kuwanasa baadhi ya watu, huku kukiripotiwa idadi ya watu wengi waliojeruhiwa katika nchi jirani ya Syria.

Kitovu cha tetemeko la Jumatatu kilikuwa katika mji wa Defne, katika mkoa wa Uturuki wa Hatay, eneo lililoathirika vibaya katika tetemeko la Feb 6 la kipimo cha 7.8.

Tetemeko la Jumatatu lilisikika pia nchini Syria, Jordan, Cyprus hata nchini Misri, likifuatiwa na tetemeko la pili la kipimo cha 5.8.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Suleyman Soylu amesema watu watatu waliuawa na 213 kujeruhiwa.

Juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa manusura zilikuwa zikiendelea katika majengo matatu yaliyoporomoka ambako watu sita wanasadikiwa wamenaswa.

XS
SM
MD
LG