Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:38

Tesla imepunguza bei ya magari yake yanayotumia umeme Marekani na Ulaya


Kampuni ya magari ya Tesla
Kampuni ya magari ya Tesla

Bei ya chini katika masoko makubwa ya Tesla inaashiria kurudi nyuma kutoka kwa mkakati ambao mtengenezaji wa magari alikuwa amefuata kupitia sehemu kubwa ya mwaka 2021 na 2022 wakati uagizaji wa magari mapya ulipoongeza usambazaji

Kampuni ya Tesla (TSLA. O) imepunguza bei kwenye magari yake yanayotumia umeme nchini Marekani na Ulaya kwa kiasi cha asilimia 20, na kuongeza mkakati wa punguzo kubwa baada ya kukosa makadirio ya Wall Street ya utoaji wa huduma kwa mwaka 2022.

Hatua hiyo ambayo ilisababisha kushuka kwa asilimia 4.5 ya hisa za Tesla katika biashara ya kabla ya soko la Marekani ilikuja baada ya Mkurugenzi Mtendaji Elon Musk kuonya kuwa matarajio ya kudorora kwa uchumi na viwango vya juu vya riba inamaanisha kuwa inaweza kupunguza bei ili kuendeleza ukuaji wa kiasi kwa gharama ya faida.

Bei ya chini katika masoko makubwa ya Tesla inaashiria kurudi nyuma kutoka kwa mkakati ambao mtengenezaji wa magari alikuwa amefuata kupitia sehemu kubwa ya mwaka 2021 na 2022 wakati uagizaji wa magari mapya ulipoongeza usambazaji. Musk alikiri mwaka jana kwamba bei zimekuwa "za aibu" na zinaweza kuathiri mahitaji.

XS
SM
MD
LG