Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:39

Teknolojia kuwakumbusha wagonjwa wa ukimwi kufuatilia matibabu


Hii ni moja ya dawa mbalimbali zinazotumiwa kupambana na ukimwi.
Hii ni moja ya dawa mbalimbali zinazotumiwa kupambana na ukimwi.

Wanasayansi 16 kutoka bara la Afrika wameshiriki katika shindano la kutafuta ufumbuzi kwa changamoto kubwa zaidi zinazoikumba jamii katika bara la Afrika. Shindano hilo limefanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda.

Kwa muda wa miaka mitatu sasa, timu hii imekuwa ikiunda programu ya simu kwa ajili ya wagonjwa wa ukimwi.

Joel Gasana, kiongozi wa timu hii, ni mwanafunzi wa matibabu katika chuo kikuu mjini Kigali.

Amesema kuwa progamu hiyo ya simu, itawasaidia wagonjwa wa ukimwi kufuatilia matibabu yao.

Mwanateknolojia Joel Gasana ambaye ameunda programu hiyo (app) anasema :“Nchini Rwanda, viwango vya maambukizi ya ukimwi vipo juu sana, asilimia 3.3 ya idadi ya watu wameambukizwa.

Utafiti uliopo unaonyesha kwamba asilimia 27 ya watu walioambukizwa, hawazingatii matibabu inavyohitajika. Hiyo ndio sababu iliyonifanya kuunda program hii ili kuhakikisha kwamba wagonjwa wote wanazingatia matibabu”

Gasana ameongeza kuwa: “Kongamano hili limeniinua sana. Programu yangu imekubaliwa na wizara ya afya na kituo cha biolojia cha Rwanda. Tutakutana na maafisa wiki ijayo ili kuanzisha ushirikiano.”

Timu hii imechaguliwa kushiriki katika mashindano ya tuzo la uvumbuzi la jukwaa la Einstein, mwaka huu nchini Rwanda.

Jukwaa lijalo la Einstein, linatajwa kuwa kubwa Zaidi, na litawaleta pamoja wanasayansi kadhaa kutoka barani Afrika watakaojadili uvumbuzi na jinsi ya kutatua changamoto zinazolikumba bara la Afrika.

Wakati akifungua sherehe hiyo Rais Paul Kagame alisema, “Kwa mda mrefu, bara la Afrika limekubali kuachwa nyuma lakini hali hii imeanza kubadilika jinsi tunavyoona katika jukwaa hili”

Naye Dr Rose Mutiso, ni mwana teknolojia kuhusu nshati safi amesema, “nadhani ni jambo la kufurahisha na kuchochea kuona kwamba jamii hii ipo, inakua pamoja na kwa ushikamano na tupo sehemu ya jamii ya wanasayansi wa kimataifa”

Joel ameiambia VOA kuwa anaifanyia majaribio kazi ya uvumbuzi wake.

Amesema: “Nakaribia kumaliza uvumbuzi wangu. Naomba mnitakie kila la heri”

Baada ya siku tatu za kongamano na madajiliano kati ya wanasayansi hawa, ni wakati sasa wa kumaliza mashindano haya kuhusu uzinduzi wakisayansi.

Conrad Tankou, kutoka nchini Cameroon, amezindua mradi ya kisasa wa kuwasaida wanawake wanaougua saratani ya uzazi.

Rachel Sibande kutoka Malawi naye ana uzinduzi wa kutengeneza nguvu za umeme kutoka kwa mahindi.

Conrad, kutoka Cameroon, ameibuka mshindi na kutunukiwa dola 25,000 na kusema:

“Ningependa kusema kwamba hii ni mara ya kwanza programu hii inafanya natambuliwa”

Jukwaa limekamilisha kongamano hilo wakati washirika wakiwa wenye furaha tele na ahadi ya ushirikiano wa kudumu ili kuendeleza sayansi na teknolojia kote barani Afrika.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington DC

XS
SM
MD
LG