Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:03

Tatizo la maradhi ya mgongo wazi na ulemavu wa watoto


 Watoto wenye tatizo maradhi ya mgongo wazi huko Conakry.
Watoto wenye tatizo maradhi ya mgongo wazi huko Conakry.

Wataalamu wa afya duniani wanakadiria kuwa kwa kila watoto elfu wanaozaliwa mmoja huzaliwa na tatizo la kichwa maji ama mgongo wazi.

Takriban watu laki 750,000 wana maradhi ya kichwa maji , huku 160,000 wakifanyiwa upasuaji na kuwekwa mirija maalum iitayo shunt kila mwaka kote ulimwenguni, kama inavyoelezwa na mtandao wa madaktari wa Medscape (emedicine.medscape.com).

Pia watoto wachanga na vijana chini ya umri wa miaka 18 , idadi yao 56,600 wako na shunt kichwani.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA amezungumza na Emmy Taps ambaye ni muuguzi katika kitengo cha upasuaji katika hospitali kuu ya pwani, ambaye anao uzoefu wa kushughulikia watoto walio na matatizo haya kwa miaka 10 sasa.

Kwa mujibu wa muuguzi huyu mbali na mama kukosa lishe bora na matumizi ya dawa aina ya Folic Acid, ugonjwa wa uti wa uti wa mgongo na maambukizi katika ubongo hasa kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja, kuvuja damu katika ubongo wakati wa kujifungua ama mara tu baada ya kujifungua, kuumia kabla kujifungua, wakati na baada ya kujifungua.

Dalili za maradhi hayo kwa watoto wa chini ya mwaka mmoja ni, kichwa huwa kikubwa kupita kiasi, Utosi kuvimba, Macho ambayo huonekana kwa nadhari kuangalia chini. Pia Mtoto hukereka haraka (irritability), Dege dege, Fuvu kutofunga vizuri, Kutapika na Kuwa na usingizi kila wakati.

Kutokana na changamoto za maradhi haya ambayo husababisha ulemavu, wengi ya watoto walio na kichwa maji huishi maisha mafupi, hasa matibabu yanapocheleweshwa, huku wale wa mgongo wazi huishi kwa miaka zaidi japo huishilia kuwa walemavu wa viungo.

Kadhalika mbali na changamoto za matibabu, mwandishi wetu anaripoti kuwa baadhi ya kina mama hutalakiwa baada ya kupata watoto wanaopata maradhi haya wakiyahusisha na imani za kishirikina.

Wataalam wanasema kuwa watoto wenye mgongo wazi wanapata ulemavu wa hasa miguu, na kuishilia kutumia magongo ama kiti cha magurudumu.

Emily Juma ambaye ana miaka ya 20 , alijikuta akiwa mlemavu wa miguu tangu akiwa mdogo, lakini anasema kuwa japo kuna changamoto yeye anakabiliana na hali hiyo.

Akiwa anafanya kazi za jamii na pia kusomea taaluma ya jamii na maendeleo, anawataka wazazi walio na watoto wenye matatizo kama hayo kutowatelelekeza.

Hata hivyo Muuguzi Emmy anasema kuwa wazazi wameanza kuwa na ufahamu kuhusu ugonjwa huo na wengi wanafika hospitalini kwa matibabu, na mazoezi.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Amina Chombo, Kenya.

XS
SM
MD
LG