Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:51

Tanzania yashutumiwa kuruhusu meli za Iran kutumia bendera yake


Meli za mafuta za Iran zikiwa safarini
Meli za mafuta za Iran zikiwa safarini

Inadaiwa kuwa Iran inatumia bendera ya Tanzania katika meli zake kuepuka vikwazo ilivyowekewa na Marekani na Umoja wa Ulaya

Tanzania imetakiwa kusimamisha matumizi ya bendera yake katika meli za mafuta za Iran ikiwa kama juhudi za nchi hiyo kukwepa vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa na Marekani na Umoja wa Ulaya.

Mbunge mwandamizi katika baraza la wawakilishi la bunge la Marekani, Howard Berman, mdemokrat kutoka California amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kumtaka asimamishe matumizi ya bendera ya Tanzania katika meli za Iran baada ya ripoti kuwa meli za kampuni ya usafirishaji mafuta ya Iran, NITC, zimesajiliwa kama meli za Tanzania na kupeperusha bendera ya nchi hiyo.

Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar Issa Haji Gavu amesema katika mahojiano na Sauti ya Amerika, VOA, kuwa meli hizo zilisajiliwa Zanzibar kama meli za Uingereza sio meli za Iran

Mbunge Berman amesema katika barua hiyo ya Juni 29 kuwa misaada ya Marekani kwa Tanzania itakuwa hatarini endapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Katika barua hiyo Berman anasema "inasikitisha sana kuona kuwa serikali yako imechukua hatua zinazokiuka ushirika wa kimataifa unaoshirikiana, kwa njia za amani, ikiwa ni pamoja na vikwazo vya uchumi, kubadili mwenendo hatari wa serikali ya Iran. Uamuzi wa kuruhusu NITC kutumia bendera ya Tanzania unatilia mashaka sifa za Tanzania kimataifa."

Tangu Rais Kikwete aingie madarakani miaka saba iliyopita Tanzania imekuwa ikipata misaada mikubwa kutoka Marekani katika mpango wa afya wa PEPFAR ulioanzishwa na Rais George Bush na mpango wa Millenium Challenge unaoshirikiana na nchi zinazoonyesha maendeleo duniani.

XS
SM
MD
LG