Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 10:24

Tanzania yalalama, Zanzibar yasema sawa, kuhusu MCC


Balozi Seif Ali Iddi, makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi, makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar

Tanzania imezungumzia sakata la usitishwaji wa fedha za msaada awamu ya pili kutoka mfuko wa changamoto za millenia (MCC) kiasi cha dola Milioni 472 kutokana na Tanzaia kutotimiza sifa za kupatiwa fedha hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, amesema msaada huo umesitishwa na bodi ya MCC kutokana na Tanzania kupoteza sifa.

Hii ni kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana kwa upande wa Zanzibar pamoja na utekelezwaji wa sheria ya makosa ya kimtandao.

Tanzania imesema haiwezi kulalamikia ushitishwaji wa msaada huo kwavile uamuzi wa kuzitoa na kusitisha ni wa bodi yenyewe.

Balozi Mahiga amesema kutopatikana kwa fedha hizo kutaathiri Tanzania kufikia malengo endelevu ya milenia katika miradi iliyokuwa inahusika na msaada huo hususani miradi ya nishati ya umeme

Hata hivyo Balozi Maiga , akizungumzia sualal la Zanzibar, amesema licha ya kwamba ni sehemu ya Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania lakini ina katiba yake inayojitegemea.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:15 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakati huo huo, Serekali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia makamu wake wa pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, imesema kusitishwa kwa fedha hizo si tukio la kwanza kwani wahisani waliwahi kufanya hivyo mwaka 1995.

Amesema fedha hizo hazitateteresha uendeshwaji wa shughuli mbalimbali kwa mafufaa ya Wazanzibari kwani watatumia vyanzo vya ndani kukusanya mapato yatakatotumika kwa uangalifu.

Balozi Seif Iddi ametolea mfano tukio la wahisani kusitisha misaada kwa Zanzibar mwaka 1995 ambapo serikali ilifanikiwa kuendesha shughuli zake za kimaendeleo na huduma za jamii bila athari zozote.

Amesema walikuwa wanatarajia uamuzi huo, kutokana na kuwepo kwa ishara za kusitishwa fedha hizo na sasa wamejipanga kuhakikisha hakuna kitu kitakacho simama.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:03 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

XS
SM
MD
LG