Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:44

Tanzania yaiomba DRC kusaidia kuokoa raia wake 22 waliotekwa na waasi


Wanajeshi wa FRADC kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya Mai Mai
Wanajeshi wa FRADC kwenye mstari wa mbele katika vita dhidi ya Mai Mai

Tanzania ilitoa wito Jumatano kwa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kusaidia kuwaokoa raia wake 21 waliotekwa nyara mwishoni mwa mwezi jana na waasi wa Mai Mai katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Tanzania, Mindi Kasiga, aliliambia shirika la habari la kitaifa kwamba raia hao 21 wa Tanzania, pamoja na Wakenya watatu, walikuwa wakiendesha malori yanayomilikiwa na kampuni zilizosajiliwa nchini Tanzania, walipotekwa nyara na Mai Mai, kundi la wanamgambo linalojumisha makabila mbali mbali, na ambalo limekuwa likipigana mara kwa mara na vikosi vya Kongo.

Hii si mara ya kwanza kwa madereva kutoka Tanzania kujipata mashakani nchini Kongo.

Mwezi Septemba mwaka jana, waasi wa Mai Mai walichoma malori manne na kuwateka madereva wanane wa Tanzania katika ejimbo la Kivu Kusini.

XS
SM
MD
LG