Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:16

Tanzania yabadili uamuzi wake wa kuondoa marufuku ya kusafirisha wanyamapori nje ya nchi


Picha iliyochukuliwa na ndege isiyo na rubani katika eneo la Masai Mara ikiwaonyesha wanyamapori kutoka mbuga ya kitaifa ya Serengeti, July 22, 2020. Picha ya AP
Picha iliyochukuliwa na ndege isiyo na rubani katika eneo la Masai Mara ikiwaonyesha wanyamapori kutoka mbuga ya kitaifa ya Serengeti, July 22, 2020. Picha ya AP

Tanzania Jumapili ilibadili uamuzi wake wa kuondoa marufuku yenye utata ya kusafirisha wanyamapori nje ya nchi, siku moja baada ya hatua hiyo kuzua malalamiko katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Marufuku hiyo iliwekwa mwaka 2016, ili kulinda wanyama na ndege wanaolindwa nchini humo ambao walikuwa wakisafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.

Hata hivyo Jumamosi, mamlaka ya wanyamapori ilitangaza kuwa ingeondoa marufuku hiyo kwa muda wa miezi sita kuanzia tarehe 6 Juni hadi tarehe 5 Disemba kwa wafanyabiashara kuondoa “akiba ya wanyama” ambao hawakuweza kuwauza kwa sababu ya marufuku hiyo.

Lakini katika kubadili msimamo kwa haraka, waziri wa utalii Pindi Chana aliirejesha marufuku hiyo ili kuruhusu mashauriano zaidi.

“Kulikuwa tangazo ambalo linaruhusu usafirishaji wa wanyamapori nje ya nchi lakini kama waziri muhusika, nimesimamisha hatua hiyo mara moja,” amesema.

Uamuzi wa kuondoa marufuku hiyo ulizua ukosoaji mkubwa kwenye mitandao, huku Watanzania wengi wakitaka upitiwe upya.

XS
SM
MD
LG