Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:08

Tanzania inaadhimisha siku ya uhuru kwa kufanya usafi.


Rais wa Tanzania, John Magufuli, akifanya usafi katika viunga vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania, John Magufuli, akifanya usafi katika viunga vya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Tanzania siku ya Jumatano iliadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanganyika ambayo baadaye iliungana na Zanzibar kufanya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Rais wa nchi hiyo John Magufuli aliongoza raia kwa kufanya shughuli za usafi nchi nzima.

Rais Magufuli mwenye kofia pamoja na mkewe wakifanya usafi
Rais Magufuli mwenye kofia pamoja na mkewe wakifanya usafi

Rais Magufuli alishiriki kwenye zoezi hilo la usafi katika maeneo ya kuzunguka Ikulu mjini Dar es Salaam hadi kwenye soko la samaki la feri, na kueleza kuwa ni aibu kwa Taifa kukumbwa na kipindupindu kwa sababu ya uchafu.

Miaka yote Tanzania imekuwa ikiadhimisha sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika kwa gwaride maalum la kijeshi lakini Rais Magufuli ambaye aliingia madarakani baada ya uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu aliamua watanzania washerehekee sikukuu ya uhuru kwa kufanya usafi ili kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kipindupindu.

Akiwa katika harakati za usafi, rais alipata fursa ya kuzungumza na wavuvi na wafanyabiashara ya samaki waliopo kwenye soko la feri ambalo lipo karibu na majengo ya Ikulu.

Baada ya kusikiliza baadhi ya kero za wavuvi, Rais Magufuli aliwataka wavuvi hao kuunda umoja wao ili waweze kusaidiwa, pamoja na kuwataka wavuvi kuacha kutumia mabomu au nyavu zisizokubalika.

Wakati huo huo Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mbunge wa Bumbuli kupitia Chama cha Mapinduzi-CCM, January Makamba kuhusiana na sherehe za uhuru mwaka huu ambapo alisema ndio mabadiliko ya kweli ambayo Rais Magufuli aliyaahidi wakati wa kampeni na chama cha CCM kiliahidi kufanya mabadiliko ya kweli yanayoendana na ubora wa uongozi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:09 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Alisema moja ya mambo makubwa yanayofanywa na chama tawala ni kupunguza gharama za uendeshaji, matumizi ya serikali hasa matumizi yasiyo kuwa na maana nay ale yasiyokuwa ya lazima.

January Makamba
January Makamba

Bwana Makamba alimsifia Rais Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo kwamba amefanya mambo mengi aliyoahidi wakati wa kampeni. Pia suala la kusitisha safari za nje zisizo za lazima na kuhakikisha fedha zinatumika kwa mpangilio. Alisisitiza kwamba sherehe za uhuru bado zipo lakini kilichofutwa mwaka huu ni shamrashamra zenye kugharimu fedha nyingi.

XS
SM
MD
LG