Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 03:40

Tume ya Uchaguzi Tanzania yasema iko tayari


Jaji Damian Lubuva

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imekutana na wamiliki wa vyombo vya habari Jumatano na kuwapa muhtasari wa maandalizi ya uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu

Katika mkutano huo mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mstaafu Damian Lubuva ameeleza kwamba kwa kiasi kikubwa maandalizi ya uchaguzi mkuu yamekamilika ambapo sasa wako katika mchakato wa mwisho wa kuchapisha daftari la wapiga kura baada ya kuweka hadharani lile la awali huku vifaa vingine vya uchaguzi vikiwa vimekamilika kwa asilimia kubwa.

Tume ya uchaguzi Tanzania yazungumza na waandishi
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:47 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Naye Kaimu mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi Emmanuel Kawishe aliwahakikishia wamiliki wa vyombo vya habari juu ya kuwepo na umakini wa kutosha katika uhakiki wa kura mara baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika

Tume ya taifa ya uchaguzi pia ilizungumzia kuahirishwa kwa chaguzi mbili za ubunge katika majimbo mawili ambayo baadhi ya vyama vimepoteza wagombea wao kwa kufariki dunia, katika majimbo ya Lushoto kwa CHADEMA na Ulanga mashariki kwa CCM

Ushindani mkubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uko kwa vyama viwili vya siasa vya CHADEMA chini ya mwavuli wa UKAWA na chama tawala CCM. Imetayarishwa na Dina Chahali

XS
SM
MD
LG