Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:00

Tanzania na tuhuma za rushwa: Dibaji


Kikwete.
Kikwete.

Jumatatu Disemba, 2014 Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania alitangaza uamuzi wa kumwondoa madarakani waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Professa Anna Tibaijuka, baada ya kuonekana kama alivyosema Rais Kikwete kuonekana na mgongani wa kimaslahi katika kashfa ya fedha inayojulikana kama Escrow.

Rais Kikwete alichukua hatua hiyo baada ya bunge la nchi hiyo kumtaka achukua hatua kufuatia mjadala mkubwa uliopita katika bunge hilo.

Kashfa ya Escrow ni moja ya kashfa kadha za fedha zilizoandamana uongozi wa Rais Kikwete tangu achukue madaraka mwaka 2005, katika hali ambayo tatizo la ulaji rushwa linaonekana si geni kwa Tanzania kama ilivyo nchi nyingine nyingi za Afrika. Ripoti ya taasisi ya kimataifa isiyo ya kiserikali Global Finacial Integrity imegundua kwamba mataifa maskini duniani yanapoteza fedha chungu nzima kila mwaka kutoka ulaji rushwa na mashirika ya biashara kukwepa kulipa kodi kuliko fedha kutoka mataifa fadhili.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba mataifa yanayoendelea yamepoteza jumla ya dola trilion6.6 kati ya 2003 hadi 2012. Na nchi tatu za afrika zilizoathirika sana na rushwa ni Sierra leone, Guinea na Liberia zinazopoteza dola bilioni 1 milioni 300 kwa mwaka.

Tanzania, na jirani zake kama Kenyana Uganda, zimekuwa zikitajwa mara kwa mara katika ripoti za kila mwaka za taasisi ya kimataifa ya Transparency International kwa kuwa miongoni mwa nchi zenye rushwa sana.

Tangu Rais Kikwete kuchukua madaraka mwaka 2005 serikali yake imekumbwa na kashfa kubwa tano za rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma – ingawa nyingine zilikuwa zimeanzia katika utawala uliopita wa rais Benjamin mkapa. Absalom Kibanda ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania.

Miongoni mwa hizo zilikuwa kashfa za Richmond, akaunti ya EPA, uporaji wa mali asili na hadi hii ya karibuni ya akaunti Escrow

XS
SM
MD
LG