Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:55

Tanzania yashutumiwa kwa ukandamizaji uhuru wa habari.


Hatua ya serikali ya Tanzania kuchukua hatua ya kulifuta gazeti la kila wiki la Mawio kutokana na shutuma za kuchapisha habari zenye mwelekeo wa kichochezi na kuhatarisha amani, imepokelewa kwa hisia tofauti na wadau wa sekta ya habari nchini humo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:15 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Waziri wa habari wa Tanzania, Nnape Nnauye alitangaza Jumapili kwamba gazeti hilo limefutwa milele kutokana na kuchapisha habari zenye mwelekeo wa kichochezi na kuhatarisha amani, baada ya kuonywa mara kadhaa na serikali.

Katibu wa jukwaa la wahariri nchini Tanzania Bw. Neville Meena akizungumza na VOA amesema kwamba hii inaashiria kuibuka upya kwa namna ya ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini humo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:24 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Alitoa lawama dhidi ya sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 1976 na kusema kwamba ni sheria kandamizi akiongeza kwamba hilo ni jambo ambalo halikubaliki na kilichofanywa na serikali si sawa.

Naye mmoja wa wamiliki wa gazeti hilo Mbunge wa Ubungo, Bw.Said Kubenea amesema kwa hatua hiyo ya serikali inabainisha kuwa serikali ya Magufuli imeanza vibaya katika utawala wake, alipoulizwa kuhusu maelezo ya waziri kuhusu maonyo alipinga akisema kwamba gazeti hilo halijawahi kupokea onyo hata moja kutoka serikalini.

XS
SM
MD
LG