Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:18

Madaktari wa Tanzania wagoma


Mgomo wa madaktari unawaathiri pia wagonjwa wanaotegemea kupatiwa huduma muhimu za afya

Madaktari wadai mazingira bora ya kazi, mageuzi katika wizara ya afya na kupatiwa posho nyingine zilizotolewa kinyemela

Madaktari wa Tanzania wameanza mgomo rasmi katika hospitali za rufaa pamoja na vituo mbali mbali vya kutoa huduma za afya nchini humo.

Wanasema wataendelea na mgomo wao hadi hapo serikali itakaposhughulikia matatizo yao. Madaktari hao wanamtaka pia Rais Jakaya Kikwete kufanya mageuzi makubwa katika wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Hata hivyo madaktari katika hospitali kuu ya Muhimbili mjini Dar es Salaam wanasema kazi zinaendelea katika hospitali hiyo na hakuna mgomo unaoendelea.

Madai mengine wanayoyataka ni pamoja na kuwepo mazingira bora ya kufanyia kazi, vifaa bora katika hospitali na vituo vya afya, kuboresha malipo ya posho, pamoja na kuheshimiwa kile wanachosema ni ‘kudhalilishwa taaluma yao’.

Akielezea madai zaidi wanayotaka yafanyiwe kazi na serikali ya Tanzania, Dk.Stephene Ulimboka, mwenyekiti wa kamati ya muda ya jumuiya ya madaktari, alisema kuwa kamati inasisitiza madaktari warejeshewe nyumba zao za kuishi kama inavyoeleza kwenye kanuni za serikali kuwa daktari atapatiwa nyumba ya kuishi na serikali au kama hatapatiwa nyumba basi atapatiwa asilimia 30 ya mshahara.

Dk.Ulimboka alisema kuwa kanuni hiyo iliondolewa bila wao kufahamishwa na kuwapa wakati mgumu kuweza kujikimu na maisha yanayoendelea kupanda siku hadi siku.

Kwa upande vwake Dk. Kasian Mkuwa wa hospitali ya Dodoma anasema mgomo sio tu kwa maslahi ya madaktari, lakini kwa maslahi ya wagonjwa

Na mgomo huu wa madaktari hauwaathiri madaktari pekee bali hata wagonjwa ambao wanategemea kupata huduma za afya kutoka kwa wataalamu hao na huwenda ukasababisha madhara kwa wagonjwa ikiwemo vifo vinavyotokana na uzembe au kutopatiwa matibabu kwa wakati unaostahili kutokana na kukosekana kwa madaktari.

XS
SM
MD
LG