Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:57

Bunge la Afrika Mashariki kukutana kujadili mzozo wa Burundi


Mwanjeshi Burundi
Mwanjeshi Burundi

Wasiwasi kuhusu kuzorota usalama na hali ya kibinadam huko Burundi, kumepelekea kuitishwa kwa kikao cha dharura juu ya mzozo huo na kamati ya kutatuwa mizozo ya Bunge la afrika mashariki EALA.

Kikao hicho kitafanyika katika makao makuu ya bunge hilo mjini wa Arusha Tanzania hii leo.

Makundi ya kikanda ikiwa ni pamoja na umojwa wa mawakili wa Afrika,, Jopo la mungano wa asasi za kiraia za Afrika Mashariki na chama cha mawakili cha Afrika Mashariki kwa pamoja wamewasilisha malamiko yao kwa spika wa EALA.

Mzozo huo umepekea watu wengi kufariki na kulazimisha wengine zaidi ya laki 2 kutoroka makazi yao na kwenda katika nchi jirani.

Abdallah Mwinyi, ni mwenyekiti wa kamati ya kutatuwa mizozo, anasema kundi lake linatarajia kusikiliza malamiko yalowasilishwa mbele yao, kutoka kwa makundi ya kiraia na makundi ya upinzani na kadhalika serikali ya Bujumbura. Anasema kamati yake kisha itawasilisha ripoti yake kwa bunge kamili ili kuijadili na kutowa mapendekezo juu ya njia bora ya kutatuwa mzozo wa Burundi.

Katika taarifa rasmi kwa kamati hiyo baada ya mualiko rasmi wa kushiriki, utawala wa rais wa Burundi Pierre Nkuruzinza ulisema kuwa maafisa wataweza kuhudhuria kikao hicho kuanzia Januari 18.

Bw Mwinyi, alielezea matumaini kuwa watakuja. Anasema kuwa anamatumaini mara hii serikali itapeleka maafisa kama walivyoeleza kwenye barua rasmi kwa kamati hio.

Mwinyi anasema kamati yake inaona ni muhimu kwa wadau wote kupewa fursa ya kueleza tathmini zao juu ya hali ilivyo sasa nchini Burundi. Anasema hii itawezesha kamati yake kupata tathmini halisi itakayowasilishwa baadae kwa wajumbe wa EALA.

Anasema, mpango wetu awali ulikuwa ni kupata ripoti hii juu ya Burundi kutolewa katika mkutano ujao ambao utaanza Januari 24. Lakini kabla tulipata ombi kutoka kwa serikali ya Burundi kuwa wangependa kutowa maelezo yao tarehe nyengine. Tutasubiri na kutowa fursa zote kwa serikali ya Burundi kuja na kuwasilisha maelezo yao mbele ya kamati yetu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Serikali ya Burundi hivi karibuni ilikata pendekezo la baraza la usalama la umoja wa Afrika, la kutaka kupeleka wanajeshi nchini Burundi kwenda kusaidia raia wanojipata katikati ya mapambano yanayozidisha hali ya ukosefu wa usalama nchini humo.

Hata hivyo Bw. Mwinyi anasema, ni mapema mno kwa umoja wa Afrika kupeleka vikosi Burundi, akisema, majadiliano ndio njia bora ya kutatuwa mzozo wa Burundi.

XS
SM
MD
LG