Umoja wa Mataifa umesema Jumapili kuwa Taliban kupiga marufuku dawa za kulevya nchini Afghanistan kumesababisha kushuka kwa asilimia 95 ya kilimo cha Afyuni nchini humo, ambapo hutumiwa kutengeneza Morphine na Heroin.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu ilirekodi mkataba unaokaribiana na hali jumla ya uchumi wa Afyuni kwa Afghanistan katika utafiti wake wa hivi karibuni wa kilimo cha Afyuni.
UNODC inakadiria wakulima wa Afghanistan wamepoteza zaidi ya dola bilioni 1 za mapato kutokana na mauzo ya Afyuni kutokana na kushuka kwa kasi, hali ambayo inaweza kusababisha athari mbaya za kiuchumi na kibinadamu kwa nchi maskini.
Serikali ya Taliban ilipiga marufuku kilimo cha Afyuni nchini Afghanistan, ambayo ni mzalishaji mkubwa zaidi wa Heroin duniani, hapo mwezi Aprili mwaka jana.
Forum