Katibu mkuu wa UN Antonio Guterres, amesema kwamba, “ marufuku hiyo haikubaliki wala haiwezekani”. Msemaji wa UN Stephane Dujarric amewaambia wanahabari kwamba, ”Huu ni mwenendo wa kutisha wa karibuni zaidi katika kuhujumu uwezo wa mashirika ya kutoa misaada kuwafikia wenye shida.
Katika miezi ya karibuni, Umoja wa Mataifa umeelezea wasi wasi wake kwamba marufuku hiyo huenda ikawekwa na Taliban. Januari mwaka huu, naibu katibu wa UN Amina Mohammed aliitembelea miji kadhaa ya Afghanistan kama vile Kabul, Kandahar na Herat akiandamana na ujumbe wa ngazi ya juu, ili kuzungumza na maafisa wa Taliban kuhusu hatua kadhaa zinazohujumu haki za wanawake na wasichana.
Wanawake nchini humo hawaruhusiwi huhudhuria masomo wala kufanya kazi mbali na wanakoishi.