Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:03
VOA Direct Packages

Taliban yaombwa kuzingatia haki za wanawake na wasichana Afghanistan


Mwanamke akishika bango la kulalamikia kupigwa marufuku kwa masomo ya wanawake mjini Kabul, Afghanistan, Dec. 25, 2022.
Mwanamke akishika bango la kulalamikia kupigwa marufuku kwa masomo ya wanawake mjini Kabul, Afghanistan, Dec. 25, 2022.

Mjumbe maalum wa Marekani kwa ajili ya Wanawake na Haki za binadamu nchini Afghanistan amesema kwamba jumuia ya kimataifa itaendelea kuhimiza umuhimu wa kulinda haki za wanawake wa taifa hilo.

Kwenye mahojiano na VOA mapema wiki hii, Rina Amiri alisema kwamba jumuia ya kimataifa imeweka bayana kwa utawala wa Taliban kwamba iwapo hautarejesha haki za wanawake na wasichana, hakutakuwa na maendeleo yoyote katika kurejesha uhusiano wa kawaida unaozingatiwa na utawala huo.

Amiri ambaye ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu mwingi, na ambaye amewahi kushikilia nyadhifa kadhaa kwenye Umoja wa Mataifa, pia aliwahi kuwa mshauri mkuu wa mwakilishi maalum wa Marekani nchini Afghanistan na Pakistan, Richard Holbrooke, wakati wa utawala wa Obama.

Maelfu ya wanawake walipoteza ajira zao baada ya Taliban kuchukua usukani mjini Kabul, wakati pia sera kandamizi dhidi ya wanawake zikibuniwa.

XS
SM
MD
LG