Maafisa wa Taliban nchini Afghanistan wamewakamata wafanyakazi wanne wa shirika la misaada linalomilikiwa na serikali ya Ujerumani, kulingana na wizara ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo ya Ujerumani.
Ninaweza kuthibitisha kuwa wafanyakazi katika shirika la GIZ wametiwa mbaroni ingawa hatujapokea taarifa yoyote rasmi inayohusu kwa nini walikamatwa, msemaji wa wizara hiyo aliliambia shirika la habari la Associated Press katika taarifa yake Jumamosi jioni.
“Tunaichukulia hali hii kwa umakini mkubwa na tunafanya kazi kupitia njia zote zinazopatikana kwetu ili kuhakikisha wenzetu wanaachiliwa”, aliongeza. Shirika la Ujerumani la Ushirikiano wa Kimataifa (GIZ) linamilikiwa na serikali ya Ujerumani.
Iinafanya kazi katika nchi karibu 120 ulimwenguni likianzisha miradi na huduma katika maeneo ya “maendeleo ya kiuchumi, kukuza ajira, nishati na mazingira, na amani na usalama”, kulingana na tovuti ya shirika hilo.
Taliban walichukua udhibiti wa Afghanistan hapo Agosti mwaka 2021, baada ya kuondolewa vikosi vya Marekani na NATO kutoka nchini humo. Kazi nyingi za kigeni ikiwemo Ubalozi wa Ujerumani mjini Kabul ulifunga ofisi zao.
Forum