Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:28

Taliban imewakamata watu watano kwa kujaribu kusafirisha madini kutoka Afghanistan


Mfano wa madini aina ya Lithium
Mfano wa madini aina ya Lithium

Mohammad RasoolAqab afisa mwandamizi katika Wizara ya Madini na Petroli ya Afghanistan alikadiria madini hayo "yalikuwa na hadi asilimia 30 ya lithiamu". "Yalitolewa kwa siri" kutoka Nuristan na Kunar majimbo mawili kati ya mengine ya Afghanistan yalioko kwenye mpaka na Pakistan

Mamlaka ya Taliban nchini Afghanistan imewakamata watu watano wakiwemo raia wawili wa China kwa madai ya kujaribu kusafirisha tani 1,000 za mawe yenye lithiamu nje ya nchi hiyo.

Kukamatwa na kuzuiliwa kwa madini hayo kulifanywa katika mji wa mpakani wa mashariki mwa Afghanistan wa Jalalabad.

Raia hao wa China na washirika wao wa Afghanistan walikuwa wanapanga kusafirisha kinyume cha sheria "mawe yenye thamani" kwenda China kupitia Pakistan, wamesema maafisa wa ujasusi wa Taliban katika matamshi yaliyorushwa Jumapili na vituo vya televisheni vya Afghanistan.

Mohammad RasoolAqab, afisa mwandamizi katika Wizara ya Madini na Petroli ya Afghanistan, alikadiria madini hayo "yalikuwa na hadi asilimia 30 ya lithiamu". "Yalitolewa kwa siri" kutoka Nuristan na Kunar, majimbo mawili kati ya mengine ya Afghanistan yalioko kwenye mpaka na Pakistan, aliongeza.

Watawala wa Kiislamu wamepiga marufuku uchimbaji na uuzaji wa lithiamu tangu waliporejea madarakani nchini Afghanistan hapo Agosti 2021 baada ya wanajeshi wote wa Marekani na NATO kuondoka nchini humo.

Afghanistan inaripotiwa inayo madini adimu yenye thamani ya dola trilioni moja, ikiwa ni pamoja na amana kubwa za lithiamu, lakini miongo kadhaa ya vita imezuia maendeleo ya madini nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG