Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 15:22

Taliban yateka wasafiri 17


Maafisa wa kieneo walioko Afghanistan wanasema kundi la Taliban limeteka takriban wasafiri 17 kaskazini mwa nchi jumatano jioni.

Msemaji wa Gavana wa eneo hilo, Zabiullah Amani, amesema wasafiri hao amabo ni wakazi wa wilaya ya Balkhab walikuwa wakielekea kwenye mji mkuu wa Sar e Pul wakati walipotekwa nyara.

Ameongeza kusema kuwa wazee wa kikabila wanashauriana kuhusu kuachiliwa kwao.

Hii ni mara ya pili kwa kundi la Taliban kuteka halaiki ya watu nyara katika kipindi cha wiki moja. Mapema wiki hii, kundi hilo liliteka nyara wasafiri 200 baada ya kuweka kizuizi kwenye barabara katika jimbo la kaskazini la Kunduz. Baadae waliachilia baadhi yao huku wakiuwa 17 kati yao.

Wakati huo huo, mamia ya waandamanaji wamekusanyika mapema leo mjini Kabul wakikemea utekaji nyara na mauwaji yaliotokea Kunduz.

XS
SM
MD
LG