Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 01:11

Tajiri mkubwa duniani Elon Musk anunua kampuni ya Twitter kwa kitita cha dola bilioni 44


Akaunti ya Twitter ya Elon Musk yaonekana kwenye nembo ya mtandao wa Twitter, April 25, 2022. Picha ya Reuters
Akaunti ya Twitter ya Elon Musk yaonekana kwenye nembo ya mtandao wa Twitter, April 25, 2022. Picha ya Reuters

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tesla Elon Musk Jumatatu amefikia makubaliano ya kununua mtandao wa Twitter kwa pesa taslimu dola bilioni 44.

Uuzaji huo utabadilisha kampuni kubwa ya mitandao ya kijamii inayofanya biashara ya umma na kuwa kampuni ya kibinafsi, inayomilikiwa na Musk pekee, tajiri mkubwa duniani.

Majadiliano juu ya mpango huo yaliharakishwa baada ya Musk kufichua kiwango kikubwa cha fedha wiki iliyopita kufanikisha ununuzi huo.

Hisa za Twitter zimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 5 kwenye soko la hisa Jumatatu alasiri.

Musk ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kutengeneza vyombo vya kurushwa angani SpaceX, alisema Twitter inatakiwa kuwa kampuni ya kibinafsi ili iimarishe uwezo wake kwa ajili ya uhuru wa kujieleza.

Musk amejitambulisha mwenyewe kama “mtetezi mkubwa wa uhuru wa kujieleza.”

Mfanyabiashara huyo, ambaye ni mtumiaji mahiri wa mtando wa twitter mwenye wafuasi zaidi ya milioni 83, ameandika kwenye twitter Jumatatu, “Natumai hata wakosoaji wangu wakubwa wataendelea kutumia twitter, kwa sababu hiyo ndiyo maana ya uhuru wa kujieleza.”

Mapema Jumatatu, Warepublican walishangilia taarifa kwamba Musk alikuwa karibu kufikia makubaliano na Twitter.

“Hey, @elomusk ni wiki nzuri ili kumruhusu@realDonaldTrump kutumia tena twitter,” Chama cha Warepublican kimeandika kwenye twitter.

Rais wa zamani, Donald Trump alipigwa marufuku kuutumumia mtandao huo mwezi Januari mwaka jana.

XS
SM
MD
LG