Baadhi ya wachambuzi wanasema kwamba ziara hiyo ni moja wapo ya njia za kuimarisha uhusiano uliyojengwa na Taiwan kwa mataifa ya Baltic, tangu kufungiliwa kwa ofisi ya uwakilishi huko Lithuania, miaka miwili iliyopita.
Ziara hiyo imekuja baada ya Estonia kutangaza wiki iliyopita kwamba ingeruhusu Taiwan ifungue ofisi isiyo ya kidiplomasia kwenye mji mkuu wa Tallinn, kwa lengo la kuimarisha uhusinao wa kibiashara na utamaduni kati ya mataifa yote mawili.
Kupitia taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni Novemba 3, waziri wake Margus Tsahkna alifichua kuwa baraza la mawaziri lilitadhmini namna ya kuhusiana na Taiwan kwenye kikao.
Forum