Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 21:45

Majadiliano ya Syria yahairishwa


Mpatanishi wa umoja mataifa kwa Syria Staffan de Mistura akiwa katika afisi za umoja mataifa ,Geneva, Switzerland, Feb. 1, 2016.

Umoja wa mataifa yasitisha mazungumzo ya amani ya Syria yanayofanyika huko Geneva, hadi mwishoni mwa mwezi Februari.

Umoja wa mataifa jana ulisitisha mazungumzo ya amani ya Syria yanayofanyika huko Geneva, hadi mwishoni mwa mwezi Februari. Mjumbe wa umoja mataifa Stefan De Mistura, ambaye anajadiliana na wawakilishi wa rais wa Syria Bashar Al Assad na makundi ya upinzani yanayojaribu kumpindua alitoa wito wa kucheleweshwa hadi februari 25. Wakati huohuo waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergei Lavrov alisema kuwa jeshi la taifa lake halitositisha mashambulizi ya anga huko Syria hadi makundi ya kigaidi yatakaposhindwa

Wakati akitembelea Oman, waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergei Lavrov alisema mashmabulizi yanayofanywa na Russia yanalenga kundi lenye uhusiano na Al Qaida la Jabhat al Nusra, na kusema haoni sababu kwa nini mashmabulzii hayo yanapaswa kusitishwa.

Russia imekuwa ikikosolewa juu ya kampeni yake ya mashambulizi ya anga huko Syria, huku mataifa ya magharibi yakisema, mashambulizi hayo yanalenga wapiganaji wa upinzani badala ya wanamgambo lakini . Russia inakana hilo.

Jumanne, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, John Kerry, alitoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi ya anga, na badala yake kufanyike utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kerry alisema kuwa,alizungumza na waziri mwenziwe wa Russia Sergei Lavrov siku chache zilizopita, na hususan tulijadili usitishaji wa mapigano, na alisema wako tayari kufanya hivyo, na irani imesema iko tayari nayo pia kusitishwa mapigano, kwa hiyo matarajiyo yangu ni kwamba hatuwa tulizopiga hadi kufikia hapa, haraka zitazaa matunda.

Lakini akizungumza kando ya mkutano unaodhaminiwa na umoja mataifa wa mazungumzo ya amani, mpatanishi wa upinzani wa Syria, alisema jukumu la Russia katika mzozo wa Syria, umesababisha yeye kutokuwa na imani juu ya juhudi za kuleta Amani.

Bw Mohammed Alloush,alisema kuwa hawana tatizo na mwakilishi maalum wa umoja mataifa bw. Mistura, tatizo lao ni kwa serikali hii ya kihalifu inayouwa watoto na tatizo lao ni pia, ni na Russia ambayo daima inasimama na wahalifu.

Wakati huohuo, wakati mazungumzo ya Geneva yakionekana kukwama , jeshi la Syria lilidai kupiga hatuwa zaidi kaskazini mwa Alleppo, na kuvunja ngome za waasi katika miji miwili na kutishia kukata njia za waasi za kuingiza bidhaa ndani ya mji.

XS
SM
MD
LG