Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 11:26

Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa njaa imekitihiri Madaya Syria


Mtoto alokumbwa na utapia mlo mbaya mjini Madaya, Syria
Mtoto alokumbwa na utapia mlo mbaya mjini Madaya, Syria

Umoja wa mataifa unachunguza ikiwa janga la kibinadamu lillosababishwa na watu ndani ya mji wa Syria unaozingirwa wa Madaya ni kitendo cha uhalifu wa vita au uhalifu dhidi ya binadam.

Wafanyakazi wa misaada wanasema hali ya watu walokumbwa na njaa katika mji huo ni yakusikitisha na mbaya kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 5 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Sajjad Malik mkuu wa idara ya wakimbizi ya umoja mataifa nchini Syria, anasema, hakuna mfano, wa kile walichokiona huko Madaya..

Bw Malik alisema hayo kwa waandishi wa habari , siku moja baada ya umoja mataifa kupeleka msaada kwenye mji ulokumbwa na vita na wenye wakazi takriban elfu 42, na ambao umezungukwa na vikosi vitiifu na rais wa Syria Bashar Al Assad.

Bw Malik anasema kulikuwa na ripoti za kuaminika, kuwa watu huko Madaya wanafariki kutokana na njaa.

Anasema kile walichokiona huko Madaya ni kuwa kuna watu lakini watu hao hawana maisha, anasema kile kinachotendeka Madaya, hakipaswi kutendeka katika karne hii.

Yakoub El Hillo, mratibu wa masula ya kibinadam wa umoja mataifa mjini Damascus alisema kuwa, waliona watu waliokumbwa na baridi na kukabiliwa na njaa kupita kiasi, na ambao wamepoteza matumaini kuwa dunia inajaali kuhusu hali yao.

Waasi wa Syria wanaudhibiti mji huo na majeshi ya serikali yameuzunguka na kuufunga katika hali ambayo hakuna anaeweza kukimbia.

Anasema, watu huko Madaya wanataka jumuiya ya kimataifa kufanya zaidi kunyanyuwa vikwazo vilowekwa huko Syria.

Umoja wa mataifa unasema kuwa takriban wasyria laki 4 wanaishi katika maeneo yaliyozungukwa na serikali, waasi au makundi yenye silaha. Millioni wengine wanaisho kwenye maeneo ambayo ni magumu kufikiwa na wafanyakazi wa kutowa misaada.

XS
SM
MD
LG