Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:41

Syria yadaiwa kutumia silaha za kemikali


Wakimbizi wa Syria katika kambi ya Arbil, Agosti 16, 2013.
Wakimbizi wa Syria katika kambi ya Arbil, Agosti 16, 2013.
Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya nchi za Kiarabu na White House zinataka uchunguzi ufanywe juu ya madai kwamba serikali ya Syria ilitumia gesi yenye sumu.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague ameeleza hofu yake kuu kufuatia ripoti za matumizi ya silaha za kemikali zilizouwa mamia ya wanaharakati katika kitongoji kimoja cha Damascus.Hague alisema endapo taarifa hizo zitathibitika, Uingereza itapendekeza swala hilo lijadiliwe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wanaharakati wa Syria wanasema mamia ya watu waliuawa katika shambulizi la serikali karibu na mji mkuu ambapo silaha za kemikali zilitumiwa. Serikali ya Syria imekanusha madai hayo.

Wote Uingereza na Marekani zimesema matumizi ya silaha za kemikali yatakuwa ukiukwaji wa mwisho utakaopelekea hatua kuchukuliwa dhidi ya Syria. Nayo wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imesema endapo madai hayo yatathibitishwa, itabidi jamii ya kimataifa ichukue hatua.
XS
SM
MD
LG