Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 05:02

Mazungumzo ya Syria kufanyika Jumamosi


Mji wa ulioharibiwa kwa mabomu wa Aleppo, Syria.
Mji wa ulioharibiwa kwa mabomu wa Aleppo, Syria.

Umoja wa Matiafa unasema kuwa mjumbe wake maalum kwa Syria Staffan di Mistrura amealikwa kuungana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry kwa mazunguzo kuhusu Syria.

Umoja wa Matiafa unasema kuwa mjumbe wake maalum kwa Syria Staffan di Mistrura amealikwa kuungana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry pamoja na mwenzake wa Russia Sergey Lavrov kwa mazugumzo kuhusu mzozo wa Syria yatayofanyika Jumamosi mjini Lausanne Uswizi.

Naibu wa di Mistura Ramzy Ezzeldin Ramzy amethibitisha mwaliko huo ingawa hajasema matarajio kutoka kwa mazunguzo hayo. Hata hivyo amekiri imekuwa ni wiki mbaya tangu Washington ilipositisha mazunguzo na Russia kuhusu Aleppo mashariki.

Amesema hali katika eneo hilo la Aleppo linaloshikiliwa na waasi bado ni mbaya na lazima ghasia zipunguzwe. Mji wa Aleppo umekuwa ukikabiliwa na mashambulizi ya anga kutoka vikosi vya Syria vikishirikiana na vya Russia.

XS
SM
MD
LG